Tuesday, 16 June 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihudhuria sherehe za kuukaribishwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndani ya jengo la Karim Jee Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa Iran Nchini Tanzania { ICC } Sheikh Ali Bakar akizungumza katika hafla ya kukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndani ya jengo la Karim Jee Jijini Dar es salaam. Picha na Hassan Issa – OMPR
Baadhi ya Mabalozi wa Nchi za Kiislamu waliohudhuria hafla ya kukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndani ya Ukumbi wa Karim Jee Jijini Dar es salaam. Picha na Hassan Issa – OMPR
Baadhi ya Viongozi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Dar es salaam waliopata fursa ya kuhudhuria sherehe za kuukaribishwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Picha na Hassan Issa – OMPR
Ayatollah Abbas Kaab Nasab wa Baraza Kuu la Kiislamu la Jamuhuri ya Watu wa Iran akitoa nasaha kwa waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria sherehe za kuukaribishwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan Karim Jee Dar es salaam. Picha na Hassan Issa – OMPR
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Al – Hajj Mussa Salum akijiandaa kumkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuhutubia sherehe za kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Picha na Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wakati wa sherehe za kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani Mjini Dar es salaam katika ukumbi wa Karim Jee. Picha na Hassan Issa – OMPR
Balozi Seif akiagana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Al – Hajj Mussa Salum baada ya kumalizika kwa sherehe za kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Picha na Hassan Issa – OMPR





















Balozi Seif akimuaga Mkuu wa Wilaya ya Ilala Nd.Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadiq mara baada ya kukamilika kwa sherehe za kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani. Picha na Hassan Issa – OMPR
  Press Release

Jamii inapaswa kuzidisha wema, na ukarimu ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani unaokaribia kwa kuwakumbuka maskini, mafakiri, yatima, wajane na wagonjwa ili kutoa fursa kwa waumini wa dini ya Kiisalmu kutekeleza ibada ya funga kwa moyo thabiti.
Hali hii itafanikiwa zaidi iwapo wafanyabiashara wataacha tabia ya kuongeza bei ya bidhaa zao kitu ambacho huwapa shida wafungaji Ramadhan ambao huhitaji bidhaa hizo hasa za vyakula na nguo za watoto.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa sherehe za kuubaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani zilizotayarishwa kwa pamoja kati ya Baraza Kuu la Bakwata Mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Watu wa Iran zilizofanyika katika Ukumbi wa Karim Jee Jijini Dar es salaam.
Balozi Seif alisema wafanyabiashara wakijijengea utamaduni wa kutoa unafuu wa bei za bidhaa wanazouza watakuwa wamefa wema mkubwa utakaoendelea kukumbukwa na waumini hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka waumini wa Dini ya Kiislamu kujiandaa kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kujipangia kutekeleza yote ya wajibu na sunna kama yalivyo katika mafundisho ya Dini na Vitabu vyake.
Balozi Seif Ali Iddi aliwakumbusha waumini hao kwamba funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni Ibada ya lazima kutekelezwa na kila muumini wa Dini ya Kiislamu popote pale alipo.
Akizungumzia kuhusu Taifa la Tanzania ambalo linaingia katika uchaguzi Mkuu na kura ya maoni ya Katiba Mpya mwaka huu Balozi Seif  aliwaomba masheikh na viongozi wa Dini zote Nchini kuliombea Taifa kuvuka salama na amani katika masuala hayo mawili mazito.
Amefahamisha kwamba Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani Duniani licha  ya kushuhudia baadhi ya watu wabaya wakijaribu kulitia dosari Taifa kwa kujihusisha na matukio ya kuwadhuru watu wengine , kufanya vurugu na hata kutotii sheria za nchi.
Balozi Seif alieleza kwamba Viongozi wa Dini kwa kushirikiana na Wananchi wanapaswa kuwakataa watu wa aina hiyo na badala yake waongeze nguvu ya kusaidiana na Serikali Kuu juu ya kupambana na vitendo vya watu hao wabaya ili kuendelea kudumisha amani na utulivu wan chi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alilipongeza Baraza Kuu la Bakwata Tanzania Mkoa wa Dar es salaa kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Watu wa Iran kwa kuandaa sherehe za maadhimisho ya kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Alisema utaratibu wa kuukaribishwa mwezi huo mtukufu wa Ramadhani ni jambo jema na tukufu kwa vile hutoa fursa kwa waumini kukumbushana mambo yanayopaswa kufanywa ndani ya mwezi huo wa ibada.   
Mapema Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni waJamuhuri ya Watu wa Iran         { ICC } Sheikh Ali Bakar alisema  Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umejaa neema  mbali mbali unaowafungulia zaidi waumini njia ya kheir.
Sheikh Ali Bakar alisema  katika kuheshimu neema hizo waumini wa Dini ya Kiislamu wanapaswa kuitumia Baraka hiyo katika misingi iliyosisitizwa ndani ya Dini yenyewe.
Akitoa salamu zilizoambatana na nasaha kwa waumini walihudhuria sherehe hizo za kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan Ayatollah Abbas Kaab Nasab wa Baraza la Kiislamu la Jamuhuri ya Watu wa Iran alisema Saumu ni Ibada inayomuwajibika kila muislamu kuitekeleza.
Ayatolah Abbas alifahamisha kwamba utekelezaji huo ni kigezo kama alivyosimamisha kiongozi wa waumini wa Dini ya Kiislamu Duniani Mtume Muhammad { SAW } kwa amri ya Mwenyezi Muungu mola wa viumbe vyote.
Akimkaribisha Balozi Seif kuzungumza na hadhara hiyo Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Al – Hajj Mussa Salum alitahadharisha wazi kwamba muumini anayeikimbia saumi ya Ramadhan bila ya sabau za msingi aelewe kwamba amekosa imani ya Dini.
Al – Hajj Salum alisema waumini wakweli walioshiba taqwa lazima wajiandae na maandalizi ya ibada hiyo ambayo ni nguzo ya Nne katika Nguzo Tano zinazomuwajibikia kila Muumini wa Kiislamu kuzitekeleza.
Sherehe za kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani pia zimehudhuriwa na Balozi wa Misri Nchini Tanzania Bwana Mussa Sadiq, Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa IranBwana Agha Jaffar, Kaimu Balozi wa Palestina  pamoja na baadhi ya waislamu wa Mkoa wa Dar es salaam.