Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akiangalia harakati za matengenezo ya Vitabu vya Baketi katika Kiwanda cha
Uchapaji Maruhubi wakati alipofanya ziara fupi ya Kutembelea kiwanda hicho. Kushoto ya
Balozi Seif ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu
wa Serikali Bibi Hanat mohammed Aboud. Picha na
Hassan Issa–OMPR
Mfanyakazi wa Kitengo cha Kompyuta Bibi Miza Mkiwa Jecha
akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Sampuli za picha
na majarida yanayotengenezwa na mashine za kisasa za Kiwanda hicho.Nyuma ya
Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh.
Mohammed Aboud Mohammed na Kaimu Mkurugenzi za Uchapaji Bibi Hanat Mohammed na Kushoto ya Balozi Seif n Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohammed. Picha na
Hassan Issa–OMPR
Balozi Seif akipokea baadhi ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa
Kiwanda cha uchapaji Maruhubi wakati alipotembelea kuona utendaji na matatizo
yanayowakabili wafanyakazi hao. Picha na
Hassan Issa–OMPR
Press Release
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeonya kwamba haitamvumilia mtendaji ye yote wa
Serikali au Taasisi zake za Umma
atakayebainika anazorotesha ufanisi wa kazi pamoja na kuendeleza makundi katika
sehemu za kazi.
Onyo hilo
limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali wakati
akizungumza na Wafanyakazi wa Idara ya upigaji chapa na Mpiga chapa Mkuu wa
Serikali baada ya kuangalia utendaji kazi wa fanyakazi hao katika sehemu mbali
mbali za Kiwandi hicho hapo Maruhubi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema
yapo mambo yanayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi za Umma ambayo
hayapendezi kwa vile yanazorotesha ufanisi wa kazi kutokana na baadhi yao
kupenda majungu na uvivu wa uwajibikaji.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba wapo watendaji katika Kiwanda cha
Uchapaji wenye tabia ya kuendeleza uvivu jambao ambalo linawavunja moyo wenzao
walioamua kufanyakazi kwa juhudi. Hivyo watendaji hao wanapaswa kujirekebisha
mara moja.
Alifahamisha
kwamba tabia hiyo mbaya inaiumiza Serikali Kuu iliyoamua kutumia fedha nyingi za kigeni katika kuimarisha miundo mbinu ya
kisasa ya Kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha katika kiwango chaTeknolojia ya kisasa.
“ Pamoja na
changamoto zinazokukabilini katika utendaji wenu wa kazi lakini Serikali kamwe
haitosita kumchukulia hatua mtendaji ye yote atakayeonyesha tabia ya kuanzisha
makundi na uvivu katika kazi “. Alisema Balozi Seif.
Aliwaeleza
wafanyakazi hao wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali waelewe kwamba wanawajibika katika eneo muhimu
kwa Taifa jambo ambalo wanahitajika kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu
yao ya kila siku.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alifafanua kwamba Ofisi yake inayosimamia Kiwanda
hicho iko katika matayarisho ya kuandaa Rasimu itakayoiomba Serikali Kuu
kukifanya kiwanda hicho mabadiliko ya kuwa Mamlaka inayojitegemea.
Alisema
hatua hiyo itasaidia kuiongezea mapato Taasisi hiyo yatakayokidhi huduma za
uendeshaji kamili pamoja na mafao ya wafanyakazi waoenbdesha Kiwanda hicho.
Mapema
Wafanyakazi hao walielezea changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa
majukumu yao ya kila siku ambazo zimekuwa zikichangia kupunguza ari yao ya
kjazi.
Walisema tatizo
la usafiri kwa watendaji wanaomaliza kazi nyakati za usiku limekuwa mtihani
mkubwa wa muda mrefu, posho kwa muda wa
ziada pamoja na ukosefu wa mafunzo kweza kuzimudu vyema mashine za kisasa
wanazotumia.
Akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya changamoto hizo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohammed alisema kwamba Wizara hiyo itaomba
ruhusa ya Serikali Kuu kununua Gari itakayosaidia kupunguza changamoto ya
usafiri kwa watendaji hao.
Dr. Khalid
alisema tatizo la posho za ziada kwa watendaji hao zimekuwa zikilipwa na
Wizara kwa mujibu wa maombi
yhanavyopelekwa licha ya kwamba Taasisi hiyo imekuwa ikitumia fedha za ziada za
Idara nyengine katika kununulia mali ghafi za kuchapisha kazi muhimu za Taasisi
za Serikali.
Akigusia
suala la mafunzo Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar alieleza kuwa Wizara ina mpango wa kuwapeleka mafunzoni wafanyakazi
watano wa Kiwanda hicho kwenye kwenye
mashine zinazofanana na zile wanazotumia ili wapate uzoefu.