Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar uliopo Michenzani
ukionekana kuwa katika mandhari nzuri ukiwa katika asilimia 98% ya kukamilika
kwake. Picha na Hassan Issa –
OPMR
Balozi Seif akitia saini kitabu cha wageni mara tu alipowasili katka eneo
la ujenzi wa Mrana wa Kumbu kumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Hapo Michenzani
Mjini Zanzibar.Wa kwanza
kutoka kushoto ni Mshauri Muelekezi wa Ujenzi wa Mrana huo Bwana Habib
Nour,Afisa wa ZSSF Makame Mwadini na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar Nd. Abdulwakil Haji Hafidh. Picha na Hassan Issa –
OPMR
Mshauri Muelekezi wa Ujenzi wa Mrana huo Bwana Habib Nour Kushoto aliyevaa
shati jeupe akimpatia maelezo Balozi Seif harakati za ukamilishaji wa Mnara wa
Kumbu kubmu ya Mapinduzi hapo Michenzani Mjini Zanzibar. Kulia ya
Balozi Seif ni Mkurugenzi wa Idaya ya Ujenzi
Zanzibar Mhandisi Ramadhan Mussa Bakari na Mkurugenzi wa ZSSF Nd.
Abdulwakil Haji Hafidh. Picha na Hassan Issa –
OPMR
Mshauri Muelekezi wa Ujenzi wa Mrana huo Bwana Habib Nour akimtembeza
Balozi Seif sehemu ya juu ya mnara wa Kumbu kubmu ya Mapinduzi ambapo alipata
muda wa kuangalia mandhari ya Mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa –
OPMR
Balozi Seif akiwa na Mshauri Muelekezi wa Ujenzi wa Mrana huo Bwana Habib
Nour wakifurahia mandhari nzuri ya juu ya mnara wa kumbu kumbu ya Mapinduzi ya
Zanzibar. Picha na Hassan Issa –
OPMR
Press Release
Mnara wa
kumbu kumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 unaoendelea kujengwa katika
bustani ya Majengo la Maendeleo Michenzani unatarajiwa kukamilika ujenzi wake
rasmi kati ya mwishoni mwa mwezi huu wa sita au mwanzoni mwa mwezi wa saba
mwaka huu.
Ujenzi wa mrana
huo ulioanza katika shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi mwezi
Januari mwaka 2014 una urefu wa Mita
35.5 zitakazowawezesha watu watakaobahatika kupanda juu ya mnara huo kuona
mandhari ya Mji wa Zanzibar.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kutembelea
maendeleo ya ujenzi wa Mnara ambayo yako katika hatua za mwisho kukamilika
kwake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } Nd. Abdulwakil Haji
Hafidh alimueleza Balozi Seif kwamba Mnara huo umejigawa katika sehemu tatu
zitakazojitegemea.
Nd. Hafidh
alisema sehemu ya chini itakuwa Maktaba maalum ya vielelezo vya kumbu kumbu ya
Mapinduzi ya Zanzibar itakayotowa fursa kwa wananchi kujifunza mambo mbali
mbali ya Historia ya Mapinduzi hayo.
Alisema
sehemu ya kati itatengwa maalum kwa
huduma za vyakula na vinywaji wakati ile sehemu ya tatu itakuwa maalum kwa
watakaopanda juu kuangalia mji wa Zanzibar kwa kutumia camera maalum sambamba
na Mkahawa wa Michezo { Sports Restaurent } utakaotoa nafasi kwa
vijana kujifunza mambo ya historia za wanamichezo maarufu Duniani.
Mkurugenzi
Mtendaji Hafidh alimueleza Balozi Seif kwamba eneo la bustani linakalouzunguuka
mnara huo wa Michenzani litakuwa na maeneo yaliyotengwa kwa wafanyabiashara
ndogo ndogo watakaoandaliwa utaratibu
maalum wa kuendesha biashara zao.
Ndugu
Abdulhakim Haji Hafidh alieleza kwamba ujenzi wa Mnara huo unaotarajiwa
kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 5
ambapo hadi sasa matengenezo ya mnara
huo yameshagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.8.
Naye Mshauri
Muelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa Mnara wa Kumbu kumbu ya Mapinduzi Bwana Habib Nour alimfahamisha Balozi Sei
kwamba sehemu ya juu ya mnara huo imetengenezwa kitaalamu itakayowawezesha
wananchi kupata huduma za vinywaji huku ikiwa
inazunguuka ili kuwapa raha na burdani wananchi hao.
Bwana Habib
Nour alisema mradi wa Ujenzi huo
unaotarajiwa kuzunguukwa na Bara bara ukijumuisha Camera maalum za CCTV kwa
ulinzi na usalama wa eneo hilo umefikia asilimia 95% ya ujenzi wake.