Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifungua
Semina ya siku moja ya Usafiri Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
iliyofanyika kwenye ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi Mbweni.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Juma Duni Haji akitoa
maelezo kwenye Semina ya Usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi kabla ya ufunguzi wa Senmina hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho ambae ndie
Mwenyekiti wa Semina ya Usafiri wa
Barabarani akitoa maelezo ya kumkaribisha Mgeni rasmi Balozi Seif kufungua Semina hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wadau
wa usafiri walioshioriki semina ya usafiri wa bara barani wakifuatilia Horuba
ya Mgeni rasmi Balozi Seif hayupa Pichani.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wadau
wa usafiri walioshioriki semina ya usafiri wa bara barani wakifuatilia Horuba
ya Mgeni rasmi Balozi Seif hayupa Pichani.
Mkurugenzi wa Idara ya Usafiri na Leseni Nd. Suleiman Kirobo akitoa Mada
kwenye Semina ya Usafiri wa Barabarani iliyoshirikisha wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi pamoja na wadau wa sekta ya usafiri.
Mkuu wa Kikosi cha UsalamaBara barani Kamishna Msaidizi wa Polisi
{ ACP } Nassor Ali Moh’d akitoa ufafanuzi wa ajali za barabarani zinazoonekana
kuongezeka kutokana na matumizi mabovu ya bara bara kwenye semina ya usafiri wa
bara barani.
Press Release
Viongozi
wenye fursa za maamuzi pamoja na nyadhifa katika Taasisi za Umma Nchini
wameombwa kuwaelimisha Vijana wao wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria
za usalama barabarani badala ya kuwasubiri kuwaombea wanapokamatwa na askari wa
usalama bara barani kwa kufanya makosa tofauti ambayo mengi kati yao ni yale
ya makusudi.
Akiifunguwa
Semina ya usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hapo
kwenye ukumbi wa Baraza hilo Mbweni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi alisema tabia ya baadhi ya viongozi kuwaombea Vijana wao
kuwachiliwa kwa makosa yao ya makusudi ni kuwavunja moyo Polisi na kupelekea
kuonekana hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
Balozi
Seif
alisema imekuwa ni jambo la kawaida hivi sasa kwa baadhi ya Viongozi
kuwaombea vijana wao wasifikishwe Mahakamani wakati wanapofanya
makosa jambo ambalo kwa kiasi kikubwa
linaondosha heshima yao ndani ya jamii.
Alisema
uvunjwaji wa sheria za usafiri wa barabarani unaofanywa na watumiaji wa
barabara hizo kama waendesha vyombo vya moto, gari zinazobururwa na wanyama,
baskeli na ha waendao kwa miguu husababisha
ajali zinazoleta madhara kwa
Taifa.
Balozi Seif
alieleza kwamba Serikali imejenga bara bara mbali mbali Nchini lwa lengo la
kuimarisha miundombinu ili kuufanya usafiri huo kuwa salama kwa watumiaji,
lakini kwa bahati mbaya kuimarika huko kumekuwa ndio sababu ya waenesha vyombo
vya moto kwenda mwendo wa kasi katika barabara hizo bila ya kujali watumiaji
wengine wa bara bara.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwamba hivi sasa ipo tabia ya hatari kwa
vijana waendeshao vyombo vya moto vya ringi mbili kufanya mashindano yasio
rasmi katika bara bara mbali mbali hasa zilizomo ndani ya maeneo ya Mji wakiwa
katika mwendo wa hatari wa kasi kubwa.
Alisema jamii
imekuwa shahidi iliwaona Vijana wanaoendesha Vyombo vya ringi mbili Vespa na
Pili pili wakipakizana watu zaidi ya wawili katika chombo huku wakifukuzana kwa
mwendo wa kasi wakiwa wamekaa katika mkao wao maarufu { T.
ONE } huku vyombo hivyo vikichomolewa breki kwa makusudi.
Alisema
chakusikitisha zaidi baadhi ya vijana hao huendesha vyombo hivyo kwa ringi moja
tuu vikiwa kwenye mwendo mkali bila ya hata kuvaa kofia ngumu lakini jambo la ajabu zaidi baadhi yao ni viongozi katika
Jamii hii.
Alifahamisha
kwamba matatizo ya usalama katika bara bara yanamgusa kila mwana Jamii, hivyo
ni wajibu wa kila Mwananchi kusaidia kuchangia upatikanaji wa ufumbuzi wa
kudumu ili kuifanya sekta hiyo kuwa salama kwa watumiaji wote wa Bara bara.
“ Usafiri wa
bara bara kuwa salama katika visiwa vya Zanzibar kutaimarisha uchumi wake kwa
kuitumia miundombinu ya usafirishaji ambayo inajengwa kwa kutumia fedh nyingi pamoja na kuiokoa
nguvu kazi ya Taifa inayohitajika katika uzalishaji “. Alisema Balozi Seif.
Akizungumzia
usumbufu wa tatizo la vituo vya dala dala katika baadhi ya maeneo ya Mji wa
Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar aliwaomba Wananchi kuendelea kuwa wastahamilivu wakati Serikali yao
ikiwa katika harakati za kuimarisha mpango Mkuu wa Mji wa Zanzibar.
Alisema
mp[ango huo utaweka utaratibu mzuri wa vituo vya gari za abiria utakaorahisisha
usafiri kwa Wananchi hasa wale wanaoonekana kusumbuka kwa kukosa kituo cha
uhakika cha wananchi wanaosafiri na kurejea Zanzibar kwa kutumia Bahari ambao
hulazimika kubeba mizigo yao kwa kufuata kituo cha gari masafa marefu.
Balozi Seif
alizishauri Taasisi zinazohusika na usafiri, mipango Miji na Vijiji kufikiria
njia bora za mpito zitakazosaidia wananchi kuondokana na usumbufu wanaoupata wa
usafiri hususan katika Miji ya Zanzibar.
Kuhusu tabia
mbaya ya baadhi ya madereva wenye tabia ya kuwachukuwa abiria na kutowafikisha
sehemu zilizowekwa kisheri Balozi Seif aliwashauri Wananchi kutokubali kuteremshwa njiani na ye yote
atakayefanyiwa hivyo aripoti Polisi ili Dereva atakayehusika na tatizo hilo
achukuliwe hatua za kisheria.
Alisema
limekuwa ni jambo la kawaida kwa madereva wad ala dala na hata gari za shamba
kuchukuwa abiria na kuwakatisha safari zao hali inayosababisha usumbufu mkubwa
kwa abiria hao wakati wengine wanaelekea Hospitalini.
Balozi Seif
alifahamisha kuwa gari yoyote
inayoingizwa katika shughuli za biashara inalazimika kufuata sheria na taratibu
za biashara husika kinyume chake ni kufanya makosa.
“ Dereva
anapoanza kazi ya kupakia abiria aelewe kuwa ameingia katika mkataba na abiria.
Hivyo anawajibika amchukuwe na kumfikisha hadi kituo cha mwisho cha safari
iliyopangiwa dala dala yake abiria huyo ambaye naye atawajibika kulipa Nauli
kwa huduma aliyopewa. Mmoja wao kama hakutekeleza hayo atakuwa amefanya kosa na
anastahiki kuchukuliwa hatua za kisheria “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wananchi kwambacSerikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar inaungana na Umoja wa Mataifa katika kuona kwamba ifikapo mwaka
2020 vifo vinavyotokana na ajali bara barani vinapungua kwa asilimia 50%.
Balozi Seif
alieleza kuwa katika kutekeleza hilo Serikali imeunda kamati ya Kudumu ya
Kitaifa ya usalama bara barani kama watendaji wa miundombinu, afya, Elimu,
Polisi na Jumuiya za Magari ambayo itakuwa na jukumu la kutekeleza jukumu hilo.
Mapema
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mh. Juma Duni Haji alisisitiza umuhimu wa mashirikiano ya pamoja
kwa Taasisi zote zinazosimamia shughuli
na harakati za Bara bara ndio njia pekee itakayosaidia kupunguza au kuondosha
kabisa changamoto ya usafiri wa Barabarani.
Mh.Juma Duni
alishauri kwamba ni vyema inapotokea changamoto ya usafiri wa Barabarani
washirika wa Taasisi zinazohusika na Sekta hiyo wakajenga utaratibu wa kukutana
mara kwa mara katika njia ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.
Wakitoa mada
kwenye semina hiyo ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu usafiri na
usalama Barabarani Mkurugenzi wa Idara ya usafiri na Leseni Nd. Suleiman
Kirobo, Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Msaidizi Kamishna wa Polisi ACP
Nassor Ali Moh’d pamoja na Mdau wa Sekta ya Usafiri Bwana Waziri Hashim walisema zipo sheria zilizopitwa na wakati
mabazo kutofanyiwa marekebisho ya haraka zitaendelea kuchangia matatizo
yanayopatikana katika matumizi ya usafiri wa Bara barani.
Waliitaja
tabia iliyozuka hivi sasa kwa madereva wa vyombo mbali mbali vya moto kutumia
simu za mikononi wakati wanaendesha vyombo hivyo wanalipa changamoto kubwa
jeshi la Polisi usalama bara barani katika kukusanya ushahidi wa makosa kama
hayo.
Watoa mada
hao walisema ili kudhibiti hali ya usalama kikamilifu umefika wakati kwa sasa
Bara bara za hapa nchini kulindwa kwa mitambo maalum ya kisasa ya Camera za CCTVG mfumo ambao hutumiwa na Miji mikubwa
Duniani na kuleta mafanikio mazuri.