Baadhi ya watoto walioshiriki mbio za hisani za Nusu marathoni
zilizoandaliwa katika shamra shamra za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika
zinazotarajiwa kufikia kilele chake tarehe 16/6/2015. Picha na Hassan Issa– OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi
akisalimiana na baadhi ya watoto walioshiriki mbio za hisani za Nusu marathoni
zilizoandaliwa katika shamra shamra za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika
huko uwanja wa amani mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa– OMPR
Watoto wakionyeshana ubabe wakati wa mashindano yao yam bio za Nusu marathoni
zilizoandaliwa katika shamra shamra za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.
Picha na Hassan Issa– OMPR
Picha na Hassan Issa– OMPR
Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto
Mh. Zainab Omar Mohammed akijiandaa kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kuzungumza katika shamra shamra za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa
Afrika akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.
Ali Mohammed Shein.
Picha na Hassan Issa– OMPR
Picha na Hassan Issa– OMPR
Balozi Seif akisalimiana na Mwakilishi wa Baraza la Watoto kutoka Handeni
Mkoani Tanga Mohammed Khalid kwenye hafla ya mbio za hisani za Nusu marathoni
zilizoandaliwa katika shamra shamra za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika
hapo uwanja wa amani. Picha na Hassan Issa– OMPR
Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein akitoa
zawadi kwa washiriki wa mbio za hisani za Nusu marathoni zilizoandaliwa katika
shamra shamra za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika. Picha na Hassan Issa– OMPR
Press Release
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema
kwamba ili kupata mafanikio makubwa katika kukomesha Ndoa na Mimba za Utotoni ushirikiano
wa lazima wa kupambana na kadhia hiyo unahitajika kati ya Wazazi,Serikali
pamoja na watoto wenyewe.
Alisema
elimu ya maadili inapaswa kutiliwa mkazo katika kuwapatia watoto na wzazi kwa
lengo la kupiga vita tatizo hilo linaloonekana kuendelea kudhalilisha watoto na
akina Mama na hatimae kuviza ustawi wao.
Dr. Shein
alitoa kauli hiyo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye shamra shamra za maadhimisho ya
siku ya Mtoto wa Afrika zilizoanza kwa Mbio za Hisani za nusu Marathoni.
Mbio
hizo zilizochukuwa zaidi ya saa Moja
zimeshirkisha Watoto pamoja na Wazazi na kufanyika katika uwanja wa Michezo wa Amani Mjini Zanzibar zikishuhudiwa
na wanafunzi na watu mbali mbali.
Alisema Wazazi
hawanabudi kuhakikisha kwamba wanazingatia maadili na misingi mizuri ya malezi
ya watoto yanayoambatana na mazingira yatayowapa elimu na uelewa wa kutosha juu
ya athari za mimba za utotoni.
Dr. Shein
alifahamisha kwamba mimba za utotoni na ndoa za umri mdogo ni utamaduni
unaoonekana kujengeka kwa baadhi ya Makabila na familia hapa Nchini jambo
ambalo wazazi wanapaswa kulisimamia kidete katika kulipinga kwa nguvu zao zote.
Alisema
vitendo vya unyanyasaji vinalitia aibu Taifa, ni kinyume na mafundisho ya dini
zote zinazofuatwa hapa Nchini ambapi pia ni kinyume na haki za Binaadamu na
haki za Kikatiba.
Rais wa
Zanzibar alishukuru na kuzipongeza Taasisi na mashirika ya Kimataifa na yale ya Kitaifa yanayoendelea kujitolea
kwenyea kuunga mkono juhudi za Serikali zote mbili katika kupinga udhalilishaji
wa Watoto hasa lile la kuozeshwa wakiwa na umri mdogo.
Dr. Shein
alifahamisha kwamba Serikali kupitia
taasisi mbali mbali na vyombo vya sheria
inaendelea kuhakikisha kuwa
juhudi zinaochukuliwa sasa kuimarisha ustawi wa watoto zinaleta mafanikio.
“ Mafanikio
ya pamoja ndio yatakayotuwezesha kutokomeza mimba za utotoni na ndoa za umri
mdogo. Kila mmoja aweze kutekeleza wajibu wake na kutoa mashirikiano
yanayohitajika katika kukomesha matendo hayo “. Alisema Dr. Shein.
Rais wa
Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania nay a Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikipanga na kutekeleza mipango
tofauti kwa lengo la kulinda na kuimarisha maslahi na ustawi wa watoto hapa
nchini.
Alisema
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa miongoni mwa Mataifa ya mwanzo
yaliyoridhia Mkataba wa Haki za Mtoto uliopitishwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Tarehe 20 Novembwa mwaka 1989 na kutia saini mwaka 1990.
Alieleza
kwamba katika kuhakikisha watoto wanapata heshima, fursa na haki zao
zilizobainishwa ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010- 2015 Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ilianzisha Mahakama ya watoto nchini ili kuongeza kasi
ya uendeshaji kesi na ufanisi wa kesi zinazohusiana na masuala ya watoto.
Dr. Shein
alisema Mahkama hizo zimejengwa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto ikiwa ni
pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa
watoto ambayo yatawasaidia kuweza kujieleza
sambamba na kutoa ushahidi bila ya hofu.
Alisema
Mahakama hizo zinaenda sambamba na utolewaji wa mafgunzo kupitia Mabaraza ya
Wazazi katika shehia mbali mbali juu ya malezi bora ya watoto na namna ya
kuripoti matukio ya udhalilishaji.
“ Nimefurahi
kuona kwamba leo tumezindua mtandao wa simu za huduma ya kwanza kwa wahanga wa
masuala ya udhalilishaji wa wanawake na watoto { Helpline 116 } ambao naamini
wengi wetu tunaiponga matendo machafu tulikuwa tukiusubiri kwa hamu “. Alisema
Dr. Shein.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi aliipongeza Taasisi hiyo isiyo
ya kiserikali ya C-Sema yenye makao makuu yake Dar es salaam kwa juhudi zake
ilizotoa katika kuunga mkono mapambano dhidi ya udhalilishaji wa watoto na
wanawake hapa Nchni.
Balozi wa
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za
Watoto { Save The Children } ambae ni
Mwanariadha mashuhuri wa Tanzania
aliyewika katika mbio za Kimataifa Suleiman Nyambui alionya kwamba jamii
isisubiri kuonywa au kuelekezwa juu ya kupiga vita Ndoa na Mimba za utotoni.
Suleiman
Nyambui aliendelea kukemea tabia ya baadhi ya Makabila Nchini wenye kuendeleza
mila potovu za kuwakataza watoto na wanawake kutokula baadhi ya vyakula vyenye
siha na kujenga afya ni kuwanyima kahi yao ya msingi.
Akitoa
salamu za Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Watoto { Save The Children }
Mkurugenzi wa Shirika hilo Nchini Tanzania Steve Thorne alisema kwamba juhudi
zinapaswa kuchukuliwa na taasisi tofauti kwa kushirikiana na Serikali katika
kusaidia kuondosha vifo vya watoto.
Bwana Steve
aliipongeza Tanzania kwa hatua yake iliyochukuwa na kufikia hatua ya nne katika
mapambano yake dhidi ya vifo vya watoto kwa mujibu wa mpango wa Kimataifa wa
Milenia wa kupunguza vifo hasa Barani Afrika.
Akimkaribisha
Mgeni rasmi katika shamra shamra hizo Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii,
Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Zainab Omar Mohammed alisema Mtoto za
Kizanzibari lazima akuwe salama na
kuepushwa na vikwazo ili apate nafasi ya kulitumikia Taifa lake kwa ufanisini.
Mh. Zainab
alisema katika kufanikisha hilo aliwaombna wazazi lazima watenge muda wao kwa
kucheza na watoto wao ili kukabiliana na
changamoto la mtoto kulelewa na mmzazi mmoja tu.