Thursday, 11 June 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wachezaji pamoja na Viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe { Wakombozi wa Ng’ambno } katika hafla ya kukabidhiwa Kikombe cha ubingwa baada ya Timu hiyo kupanda Daraja la kwanza Kanda mwaka huu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea Kombe  kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Moh’d Said Dimwa walilolitwaa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe { Wakombozi wa Ng’ambo } na kupanda Daraja la kwanza Kanda.
Balozi Seif akifurahia Kombe walilolitwaa Wakombozi wa Ng’ambo { Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe katika hafla fupi ya kukabidhiwa hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Moh’d Said Dimwa akielezea mitkakati iliyowekwa na Uongozi wa Jimbo lake la kuifufua Tena Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe iliyopata umaarufu mkubwa katika miaka ya hivi karibuni. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Rais wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe Salim Ridhiwani akizitaja changamoto zinazoikabili Timu yake ambayo hata hivyo iliibuka ya ushindi wa kupanda daraja la Kwanza Kanda. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Msemaji wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe Haji Khalfan Haji { Haji Kiduka } akimshukuru Balozi Seif kwa umahiri wake wa kuunga Mkono Sekta ya Michezo Nchini. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Baadhi ya Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe wakifuatilia nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani kwenye hafla fupi ya kukabidhi kikombe baada ya Timu yao kupanda Daraja la Kwanza Kanda. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe wakifuatilia nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani kwenye hafla fupi ya kukabidhi kikombe baada ya Timu yao kupanda Daraja la Kwanza Kanda. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ. 


Baadhi ya Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe wakifuatilia nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani kwenye hafla fupi ya kukabidhi kikombe baada ya Timu yao kupanda Daraja la Kwanza Kanda.  Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Press Release:- { Michezo } 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amehimiza umuhimu wa wanamichezo kuendelea kudumisha nidhamu michezoni ili kulijengea sifa Bora Taifa katika sekta hiyo kwa kuwa na wanamichezo  walishiba maadili na heshima iliyotukuka.
Balozi Seif Ali iddi alitoa himizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji pamoja na Viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe { Wakombozi wa Ng’ambno } katika hafla ya kukabidhiwa Kikombe cha ubingwa baada ya Timu hiyo kupanda Daraja la kwanza Kanda mwaka huu.
Alisema nidhamu na heshima ndio kitu pekee kilichosababisha  wachezaji wa enzi zilizopita hapa Zanzibar kuwika na hatimae kuiletea sifa Zanzibar katika ulimwengu wa kabumbu.
Balozi Seif alieleza kwamba Vijana wa sasa wana nafasi pana ya kuendelea kujifunza mbinu mbali mbali za michezo na hatimae kuwa  mastaa ambazo hupatikana kupitia kwenye vipindi vya Televisheni pamoja na mitandao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wachezji pamoja na Viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe kutokana na kazi kubwa waliyoifanya na hatimae kuchukuwa ubingwa kwa kuingia daraja la Kwanza Kanda.
Balozi Seif alisema juhudi za wachezaji hao kwa upande mwengine zimeanza hatua mpya ya kujijengea uwezo wa kupata ajira kupitia mchezo wa soka ambao unaonekana kupendwa sana Duniani.
“ Wapo wachezaji maarufu wanaochezea timu zinazotajika Duniani katika ulimwengu wa kabumbu ambapo wengine wanatokea hata mataifa ya Afrika yanayolingana kiwango cha soka na Tanzania “ Alisema Balozi Seif.
Katika kuunga mkono wanamichezo hao wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe Balozi Seif ameahidi kuisaidia Timu hiyo Seti mbili za Jezi pamoja na Mipira Minne na akawataka wajiwekee malengo zaidi ya kufanikiwa katika  fani yao hiyo kwa siku zijazo.
“ Wale Jamaa wakikuoneni mnavyolisakata soka sawa sawa kikweli watafikia hatua ya kukununueni tuu na kwa upande mwengine Zanzibar  tutakuwa na haki ya kujigamba kwamba tumetoa wachezaji wanaouwezo wa kuchezea timu za Kimataifa “. Alisema Balozi Seif.
Akizungumzia suala ya ujenzi wa Jengo la kudumu la Timu hiyo ya Taifa ya Jang’ombne Balozi Seif aliwashauri Viongozi na wachezaji hao kuanza ujenzi wa msingi na yeye atakuwa tayari kusaidia matofali kwa hatua ya kunyanyua.
Alisema uwezo wa kujenga jengo lao uko mikononi mwao ambapo viongozi wao jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kwamba wanasaidia nguvu na maarifa ili kuona malengo waliyojipangia yanakwenda hatua baada ya hatua.
Mapema Rais wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe Salim Ridhiwani alisema Uongozi wa Klabu hiyo umeamuwa kuimarisha Timu hiyo ili kurejesha heshima na hadhi ya klabu hiyo iliyopotea katika miaka ya hivi karibuni.
Ridhiwani alisema Wanachama wa klabu hiyo wanajivunia maendeleo makubwa yaliyopatikana ndani ya klabu hiyo hasa kutokana na wachezaji wa timu hiyo kuiwezesha timu yao kuyakabili mashindano makubwa ya Kombe la Mapinduzi na kutoa upinzani mkubwa kwa timu zenye uzoefu wa mashindano ya soka  Kimataifa.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mohammed Said Dimwa alisema Uongozi wa Jimbo hilo umeifufua tena Timu hiyo ndani ya Kipindi cha miaka Miwili iliyopita baada ya kufifia kutokana na changamoto kadhaa zilizokuwa zikiikabili timu hiyo katika miaka ya nyuma.
Dimwa aliahidi kwamba yeye pamoja na viongozi wenzake watasimama imara katika kuhakikisha Timu hiyo inarejea katika hadhi yake iliyopewa na wapenzi wa timu hiyo ya kuitwa wakombozi wa Ng’ambo.
Timu ya Taifa ya Jang’ombe { Wakombozi wa Ng’ambo } ilipanda Daraja na kushiriki  mashindano ya Daraja la Kwanza Kanda mwaka huu  baada ya kuifunga Timu ya Soka ya Maungani  Goli 1-0 katika mchezo wa Mwisho wa mashindano ya Ligi Daraka la Pili.