Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipata
maelezo kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV
Camera Nd. Jabir Haji Abdulla juu ya mfumo wa utendaji kazi wa mradi wa Camera
za kurikodi matukio mbali mbali ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar. Kulia ya
Balozi Sei ni Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bwana
Xie Yun Liang. Picha Hassan Issa –
OMPR – ZNZ.
Katibu wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV Camera Nd. Jabir Haji Abdulla akionyesha picha mbali mbali zinazonaswa na kurikodiwa katika maeneo mbali mbali ya Mji Mkongwe. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Mounekano wa Picha tofauti zinazochukuliwa na kunaswa katika kituo cha kuongozea Camera za CCTV Malindi Mjini Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifurahia mfumo wa Camera za CCTV unavyofanya kazi ambao amesema utasaidia kupunguza au kuondosha kabisa matukio ya uhalifu na uzembe katika bara bara za Mji Mkongwe wa Zanzibar. Picha Hassan Issa – OMPR – ZNZ.

Press Release:-
Zanzibar
inatarajia kuimarika zaidi kiulinzi na kiusalama sambamba na kuongeza mapato
yake kupitia sekta ya utalii baada ya kukamilika kwa mradi muhimu wa Kamera
za kurikodi matukio mbali mbali ya kila
siku { CCTV CAMERA } zinazofungwa katika eneo la Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Mradi huo
muhimu wa Camera uliofadhiliwa na Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa
Mawasiliano ya Kisasa ya ZTE yenye Makao Makuu yake Nchini Jamuhuri ya Watu wa China umekuja Zanzibar
kufuatia ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliyoifanya Nchini China mwisho mwa mwaka uliopita.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua Kituo
cha mradi huo { Comanding Post } kiliopo Malindi Mjini Zanzibar na kujionea
Teknolojia mpya itakayotumika katika kuziongoza Kamera hizo.
Katibu wa
Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV Camera Nd. Jabir Haji Abdulla
alimueleza Balozi Seif kwamba mradi huo unatarajiwa kuwa na Carema 300 lakini
zitakazofungwa kwa sasa ni Kamera 150 ambapo hadi sasa Kumi tayari
zimeshafungwa.
Nd. Jabir
alisema Kituo hicho kitakachokuwa chini
ya uangalizi wa Idara zote za ulinzi
Nchini likiwemo Jeshi la Polisi, usalama
wa Taifa, KMKM hivi sasa tayari kina uwezo kamili wa kurikodi matukio mbali
mbali yanayotokea katika eneo la Mji Mkongwe.
Katibu huyo
wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa mradi huo alieleza kwamba Kamera za
mradi huo zenye uwezo wa kuvuta tukio kwa zaidi ya mita 150 zitasaidia kurikodi
matukio mbali mbali kama ujambazi, makosa ya bara barani yanayofanywa na
madereva wazembe pamoja na kuongoza misafara ya viongozi wakuu.
Alifahamisha
kwamba
katika kuimarisha hali ya usalama ndani ya Mji wa Zanzibar upo mradi
mwengine unaotarajiwa kusimamiwa na Kampuni ya Zest
utakaohusisha maeneo ya Bagharesa, Mlandege pamoja na Majengo ya Nyumba
za
Maendeleo Michezani.
“ Kamera
hizi zenye uwezo wa kuzunguuka pembe zote { 360% } zina uwezo wa kuvuta tukio lolote kwa zaidi ya
Mita 150 na kuwa na vigezo vya kuufanya mji salama “. Alifafanua Katibu huyo wa
Kamati ya Wataalamu ya Usimamizi wa CCTV.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliipongeza Kampuni ya ZTE kwa jitihada ilizochukuwa za kutekeleza kwa vitendo
ahadi iliyompa kuanzisha mradi huo wakati
wa ziara yake Nchini China.
Balozi Seif
alisema Serikali ilipaswa kuwa na mradi huu muhimu kwa muda mrefu uliopita hasa
ikilinganishwa na matukio mbali mbali yaliyowahi kutokea hapa nchini likiwemo
la hujuma dhidi ya wageni wanaotembelea katika maeneo ya Utalii.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea matumaini yake kwamba mradi huo kwa kiasi
kikubwa utakapokamilika utasaidia kupunguza matukio tofauti ya uhalifu,
ujambazi pamoja na ajali za kizembe zinazotokea bada barani.
Mradi wa Kamera za
kurikodi matukio mbali mbali ya kila siku { CCTV CAMERA } ndani ya Mji
wa Zanzibar umeripotiwa kuwa wa mwanzo kuwekwa ndani ya ukanda wa Afrika
Mashariki.