Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana
na Wazee na Viongozi wa Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ kabla ya kuzungumza nao kujadili
tatizo la migogoro ya Ardhi. Picha Hassan Issa–
OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati wa kujadili changamoto zinazowakabili za migogo ya Ardhi { Hifadhi ya Misitu } ndani ya Shehia hizo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kusini Bi Kibibi Mwinyi Hassan. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.
Baadhi ya Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati wa kujadili changamoto zinazowakabili za migogo ya Ardhi { Hifadhi ya Misitu } ndani ya Shehia hizo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kusini Bi Kibibi Mwinyi Hassan. Picha Hassan Issa– OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akizungumza na Wazee na Viongozi wa Muyuni “A “ na Muyuni “ B
“ baada ya kupokea changamoto zinazowakabili za migogoro ya ardhi. Kulia ya
Balozi Seif ni Mkuu wa Mkopa wa Kusini Unguja Dr. Idriss Hijja na Kushoto yake ni Mwenyekiti wa Kikao
hicho Diwani Mstaafu wa Muyuni Bwana Abdulla
Hija Abdulla. Picha Hassan Issa–
OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar haipendelei kuona Wananchi katika baadhi ya shehia
wanalumbana na kufikia hatua ya kuhitilafiana katika mambo ambayo wakiamua
kukaa pamoja katika kuyajadili kwa njia ya vikao yanaweza kurekebishika bila ya kutumika nguvu
za Serikali Kuu.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza
na Wazee na Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “B” katika kikao cha
kujadili matatizo yaliyojitokeza baina ya Wananchi dhidi ya viongozi wao wa
shehia hizo.
Balozi Seif
Ali Iddi alisema tabia ya baadhi ya wananchi hasa Vijana kutumia njia ya mkato
katika maamuzi yao ya kurejesha Kadi za
uanachama ni udhaifu unaofa kuepukwa kwa vile hauwezi ukatoa suluhu ya tatizo
linalolalamikiwa na Wananchi hao.
Alisema maisha
ya amani na utulivu ndio yanayotegemewa
na Serikali Kuu kuendelea kushamiri ndani ya Shehia hapa nchini ambazo
zinawajibika kufanya kazi kwa umakini.
Balozi Seif
alieleza kuwa Sheha wa Shehia yoyote ile
hapa Zanzibar ni mtumishi wa Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar
asiyepaswa kuhusika na vitendo vinavyoashiria vurugu ndani ya eneo lake.
Mapema Diwani Mstaafu wa Wadi ya Muyuni Bwana Abdulla
Hijja Abdulla ambae ndie mwenyekiti wa Kikao hicho alielezea matatizo mengi
yanayowasumbuwa Wananchi hao wa Muyuni “
A “ na Muyuni “ B “ hasa lile la hifadhi ya msitu ambalo waliamuwa kuianzisha kwa
hatma yao ya baadaye.
Bwana
Abdulla alisema uchelewaji wa kuchukuliwa hatua
za kisheria katika ngazi za Shehia, Wilaya na Mkoa dhidi ya watu waliomua kuvamia hifadhi hiyo ndilo
tatizo kuu lililoibua mtafaruk kati ya Wananchi hao wa Uongozi wa Shehia hizo.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Kusini Nd. Khamis Jabir Makame alisema alilazimika kulitembelea eneo
la Mgogoro wa Ardhi katika eneo la Hifadhi ya Muyuni muda mfupi uliopita ili kujionea hali halisi
ya kile kinacholalamikiwa.
Nd. Jabir
alikieleza kikao hicho kwamba akiwa pamoja na Viongozi wenzake wa Wilaya alibaini
kuwepo kwa miti ya kudumu iliyooteshwa kwa muda mrefu katika eneo hilo pamoja
na Miti ya matunda ambayo tayari imeaanza kuzaa.